31 Januari 2015 - 19:54
 Wanajeshi 15 wauwawa Mashariki mwa Ukraine

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Stepan Poltorak amesema mapigano kati ya waasi wanaoiunga mkono Urusi na wanajeshi wa serikali ya Ukraine Mashariki mwa nchi hiyo yamesababisha mauaji ya wanajeshi 15 huku wengine 30 wakijeruhiwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Stepan Poltorak amesema mapigano kati ya waasi wanaoiunga mkono Urusi na wanajeshi wa serikali ya Ukraine Mashariki mwa nchi hiyo yamesababisha mauaji ya wanajeshi 15 huku wengine 30 wakijeruhiwa ndani ya saa 24 zilizopita. Idadi hiyo ni kubwa na pigo kwa jeshi la Ukraine tangu kutiwa saini kwa makubaliano yanayoyumba, ya kusitisha mapigano huko  Minsk mwezi Septemba mwaka uliopita. Mapigano yanasemekana kupamba moto karibu na eneo la kimkakati la Debaltseve ambacho ni kitovu cha usafiri , kilomita 50 Kaskazini Mashariki mwa mji unaodhibitiwa na waasi wa Donetsk. Wawakilishi wa serikali ya Ukraine, Urusi, shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya na waasi wanaoiunga mkono Urusi wamekusanyika mjini Minsk katika jaribio la kufufua mazungumzo ya kutatua mgogoro wa Ukraine.